Kitabı oxu: «Jinsi Ya Kupata Mme»
Jinsi Ya Kupata Mume
EMMANUEL SMITH
Kimetafsariwa Na: Emmanuel Satongima
Hakimiliki © 2021 Emmanuel Smith
KUHUSU MWANDISHI
Emmanuel Smith ni mwandishi Nguli na Mzungumzaji wa hadhara.
YALIYOMO
Utangulizi
Anaonekanaje?
Unaonekanaje?
Unahitaji kwenda kutafuta.
Usijionyeshe mkali sana.
Baki kuwa wewe.
Onyesha shauku yako.
Mfanye acheke.
Ongea kidogo, sikiliza sana.
Tengeneza urafiki na marafiki zake…………………………………………………20
Jihusishe na vitu anavopenda.
Endelea na maisha yako.
Mtulize……………………………………………………………………………………………23
Usimtumie kwa manufaa yako.
Ni rafiki au mume?
Ni mwanaume wako, au mama ushauri wake?
Usijihujumu mwenyewe.
Anahitaji kuwa mume wako?
Pima shauku yake kuhusu Ndoa.
Onyesha kujali Shughuli zake.
Onyesha unajali masuala yako ya kifedha .
Kuwa mwanamke wa kawaida.
Usiharakishe mambo.
Punguza matarajio yako.
Ruhusu Uhusiano wako kukua.
Kimsingi acha kutavuta.
Utangulizi
Habari! Hongera kwa uamuzi wa kumtafuta mwenzi wa Maisha. Kwasababu unasoma kitabu hiki, ninaamini umeona ni kitu sahihi kufanya.
kwanini unahitaji mume sio kitu muhimu kwangu, wala kwa mtu mwingine yoyote. Inawezekana ni kwa ajili ya kujiongeza sifa kwenye maisha, baadhi yao ni kupata msaidizi ndani na nje ya nyumba, kwa wengine, uhitaji wa kuanzisha familia, na sababu nyingine nyingi. Kitabu hiki sio kwa ajili ya kuchambua sababu ulizonazo. Bali ni kusaidia ushauri wa namna ya kufanya matamanio yako kuwa kweli.
Ninafahamu hauna muda wa kusoma vitu vingi vitakavyokupa hasira. Kwahiyo, twende tulimalize hili, nina matumaini chini ya dakika 60 tutakuwa tumemaliza.
Anamuonekano upi?
Njia nzuri, ni kuwa na picha sahihi, ya kile unachokihitaji. Sawa, inaweza kusomeka kama kichekesho kwako, lakini kama hufahamu unachokihitaji utafahamu vipi kwamba ni hiki pindi utakapokipata. Aah, Ngoja nisikuchanganye; tufanye mazoezi ya machache ya akili pamoja.
HADITHI KUHUSU WANAUME:
“Wanaume wote ni sawa.”
Picha hii ni mbaya kama kusema wanawake wote ni sawa. Ikiwa hauamini moja ya mapendekezo haya kwa nini uamini nyingine? Na ikiwa unaamini mawazo yote mawili, basi unaweza kuwa na tumaini dogo la uhusiano mzuri. Pengine wanaume huja na tabia nyingi binafsi kama ilivyo
watu duniani.
Tengeneza picha ya muonekano wa mwanaume wa ndoto zako kwenye akili yako.Kwanini ni muhimu?Labda kama unaharaka na utachukua mwanaume wowote aliekuepo mbele yako, la kama si hivyo basi inakubidi kufanya haya.Vinginevyo, kitabu hiki si kwa ajili yako.Acha turahisishe zoezi.Kaa chini, chukua peni na kipande cha karatasi na ujiambie mwenyewe kuhusu mwanaume, mwenye bahati ambae karibuni atakuwa mume wako, Awe na muonekano upi.Furahia kuelezea sifa zake muhimu.Ufuatao ni Muongozo mfupi wa kuanzia:
Umri- Awe na umri gani?
Urefu na upana – Mrefu kiasi gani na upana wake katikati?
Aina ya maisha – Ni mpenda kuwa nje au ndani anazingatia lishe au anakula kila kitu, n.k.?
Anaishi wapi – Awe anaishi mji mmoja na wewe au mbali kwenye jiji la ndoto zako upande mwingine wa dunia?
Amezaliwa wapi – Ni mzaliwa wa nchi yako au mgeni?
Ukabila – Kama hili ni muhimu basi usipuuzie swali hili.
Dini- Ni mtu anaeamini au asieamini katika Mungu?
Elimu- Ikiwa ni sifa muhimu kwako usidharau. Kuishi na mtu aliekuzidi sana kiwango cha elimu au utashi yaweza kuwa changamoto.
Anafanya kazi gani?- Ni fundi, ofisini, au mfanyabiashara?
Kipato- kipato chake cha chini kiwe kiasi gani?mapenzi yanahitaji fedha, hata kwa kiasi kidogo kwa ajili ya chakula cha usiku pamoja, mara moja moja.Ndoa ni jambo zito hasa mnapoanza kupata watoto.
Atapenda kuanzisha familia? - Kiuhalisia ndio!huna muda na wapoteza muda.
Anavuta sigara na kwa kiwango gani? - Usianzishe mahusiano, iwapo huwezi kuvumilia mvutaji.
Anakunywa pombe na kwa kiasi gani? - Hatumii kilevi, anatumia mvinyo kiasi, au mlevi wa kupindukia mwisho wa wiki?
Pulsuz fraqment bitdi.