Kitabı oxu: «Lucilla Akiwa Mawinguni»
Table of Contents
Copertina
titolo
copyright
contenuto
Maria Grazia Gullo - Massimo Longo
Lucilla
ndani ya Mawingu
Imetafsiriwa na Emmanuel Satongima
Hakimiliki © 2019 M.G.GULLO-M.LONGO
Picha za kwenye gamba la kitabu, Ufafanuzi na michoro ilitengenezwa na kuhaririwa
na Massimo Longo na Lucia Longo
Kwa msaada wa Alfio Longo
Haki zote zimehifadhiwa.
Lucilla
Akiwa Mawinguni.
Siyo mara moja, bali mara elfu moja mama yake alisema binti asisumbuliwe anapofanya kazi za nyumbani.
Shuleni Luccilla alikuwa ni binti mwenye akili na bidii. Kila mara kichwa chake kilikuwa kwenye mawingu.
Pindi mama yake alipomkabizi zoezi muhimu kwenye mikono yake, binti aliweza kubugiziwa na kuacha nusu ya kazi haijakamilika.
Alikuwa ni binti mwenye macho ng’aavu, mwenye nywele ndevu mpaka kwenye mabega.
Kwa umri wake, alikuwa mrefu na mwembamba achilia mbali usumbufu wote aliokuwa akiusababisha, mara zote alikuwa akileta furaha katika nyumba yao.
Lucilla na familia yake waliishi kwenye kilima ndani ya msitu; walikuwa na utajili wa furaha ila masikini sana wa mali.
Hata hivyo, hiyo haikuwafanya washindwe kuwa binadamu wenye ukarimu na kuacha kumuhudumia bibi kizee aliyeishi upande wa pili wa kilima.
Miaka mingi kabla, alipokuwa kijana, bibi kizee alimlea mama yake na Lucilla, aliyekuwa yatima.
Alikuwa kama bibi kwa Lucilla. Katika kipindi hicho, bibi Tina alikuwa hajisikii vizuri: Alikumbwa na baridi ya homa.
Mama yake Lucilla ambaye kuanzia sasa tutamuita kamomile (mti ambao maua yake meupe na njano hutumika kutengeneza chai) kwa uvumilivu wake, enzi hizo ilikuwa inachosha kwenda kumtembelea bibi Tina.
Kwa hiyo, aliamua ni muda wa kulikabizi jukumu kwa Lucilla.
Pulsuz fraqment bitdi.